Monday, October 13, 2014

NGUMI KALI KUPIGWA OCTOBA 25 KATIKA UKUMBI WA FRIENDS CORNER MANZESE


Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika
October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi'  na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver  na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatuampaka kujua kitu kamili katikamchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd  Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Kwa Hisani ya :-

Wednesday, October 1, 2014

SIKILIZA NA KUPAKUA WIMBO MPYA WA METTY Ft CONRAD - NAJUA

Chek HAPA- http://www.hulkshare.com/sulejr/metty-najua-1 kupakua wimmbo mpya wa Metty - NAJUA. Ngoma imefanyika katika studio za Cenrirc Record akiwa amemshirikisha msanii Conrad. kwa mahojiano/mawasiliano zaidi check na Metty kwa nambari +255 714796622 powered by www.mtotowakitaa.blogsport.com

Wednesday, September 3, 2014

TAARIFA YA MSIBA WA BAHATI MWAKABUNGU (MWANAFUNZI WA CBE - DAR)

MAREHMU BAHATI MWAKABUNGU ENZI ZA UHAI WAKE
 
WANAFUNZI AMBAO TUMEPITA CHUO CHA BIASHARA KITUO CHA DAR ES SALAAM (CBE) TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA ALIYEKUWA MWANAFUNZI MWENZETU BAHATI MWAKABUNGU AMBAYE AMEFARIKI JUZI HAPA DAR ES SALAAM.
 
MSIBA UPO KWA KAKA YAKE NOEL MWAKABUNGU MAENEO YA BUZA JIJINI DAR ES SALAAM, TAARIFA KUTOKA KWA WANA FAMILIA WANASEMA MAZISHI YATAFANYIKA LEO TAREHE 3/09/2014 KATIKA MAKABURI YA KINONDONI MUDA WA ALASIRI.
 
KWA TAARIFA ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NA NAMBA HII:
 
0718277409
 
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Monday, August 25, 2014

MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI YAENDELEA VIWANJA VYA MASHUJAA MJINI DODOMA

Baadhi ya akina mama wakiwa wanaangalia moja ya bidhaa za katika mabanda ya wajasiriamali hao yanayoendelea hivi sasa.

Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo (Kulia) akipata maelezo ya moja ya banda linaloonyesha na kuuza bidhaa zake  za madishi na vifaa vya umeme, kwenye maonesho ya biashara za wajasiriamali yanayoendelea katika viwanja vya Mashujaa, mjini Dodoma.
Baadhi ya wateja wakichagua moja ya bidhaa za dvd na cd zinazouzwa kwenye mabanda hayo.

Na Andrew Chale, Dodoma.
MAONESHO ya wafanyabiashara kipindi cha Bunge la Maalum la Katiba yanaendelea kwa kasi mjini hapa na kuwakutanisha wajasiriamali zaidi ya 100 katika viwanja vya Mashujaa.
Akizungumza Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo, alisema lengo kuu la maonesho hayo ni kutoa fursa kwao kuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.
“Mpaka sasa tuna wajasiriamali 100,  ambao wanaendelea na maonesho  yao kwenye viwanja hivi vya Mashujaa kuanzia Agosti 10 mwaka huu, na maonesho yataendelea mpaka litakapomalizika Bunge la Katiba, hivyo bado tunaendelea kupokea wajasiliamari wengine zaidi,” alisema Dk. Kifimbo.
Alisema kuwa maonesho hayo yanajumuisha wauzaji wa bidhaa za tiba mbadala, bidhaa za majumbani, kazi za mikono kutoka ndani na bidhaa zingine mbalimbali.
Kifimbo ambaye ni mganga wa tiba mbadala alisema maonesho hayo yatazinduliwa rasmi Agosti 21, mwaka huu, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki.
Lengo ya maonyesho ni kutoa fursa kwakuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.

Thursday, August 14, 2014

MAZISHI YA MAMA TUNDA (MKE WA MSANII AFANDE SELE) YAMEFANYIKA LEO MJINI MOROGORO

UO
Professor Jay amesafiri hadi mkoani Morogoro kwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa msanii mwenzake Afande Sele.

xxxxxx

Kupitia Instagram, Professor ameshare picha akiwa kwenye mazishi na kuandika: Msibani Morogoro nyumbani kwao marehemu Asha au mama Tunda sasa hivi… tunajiandaa kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele saa kumi jioni ya leo, bwana alitoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe….Amen
Awali Afande Sele alisema kifo cha Mama Tunda kimetokana na uzembe wa madaktari. Mama Tunda alifariki baada ya kulazwa kutokana na kuugua Malaria. Akizungumzia tukio hilo, Afande alidai kuwa bila uzembe wa madaktari huenda malaria isingechukua uhai wa Mama Tunda.
“Mama Tunda ametuachia pengo kubwa sana kwenye familia,” alisema Afande. “Amefariki jana saa tano usiku katika hospitali kubwa hapa Morogoro kutokana na uzembe wa madaktari. Walimpa matibabu akarudi nyumbani, sitaki kulizungumzia kiundani kwa sasa hivi kwa sababu tupo kwenye wakati mgumu. Huku mazishi yatafanyika kuanzia kama saa tisa hivi lakini bado hatutajua itakuwa wapi bado tupo kwenye mipango. Malaria ilimchukua sana, kwa familia na watoto kwetu ni msiba mkubwa sana, yaani ni huzuni sana,” aliongeza.

Wednesday, August 13, 2014

NILIJITOA MAISHA YANGU KWENYE MUVI YA MSHALE WA KIFO - AISHA BUI


Na Mwandishi Wetu
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Asha Bui, amedai kuwa alijitoa maisha yake kutoka na filamu yake ya Mshale wa Kifo, kutokana na sinema hiyo kutengeneza porini katika msitu hatari wenye wanyama wakali.
Msanii huyo amedai alifanya hivyo kufuatia maoni ya wapenzi wa filamu ambao kila siku wanalalamika kwa kusema kuwa filamu zetu nyingi zimekuwa za mijini tu, huku baadhi ya matukio yakirudiwa kila katika sinema hizo jambo ambalo limekuwa likiongelewa mara kwa mara.
“Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, lakini najua na deni kwa wapenzi wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila mwaka,”anasema Aisha .
Filamu ya Mshale wa Kifo Imetengenezwa na Yuneda Entertainment na imewashirikisha wasanii nyota kama Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Aisha Bui, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ na wasanii wengine 

Monday, August 11, 2014

(Audio) Wille - Uze Mbela

Cheki na hii link kusikiliza na kupakua wimbo huu 

PSPF YAFUNGA NANENANE LINDI KWA KISHINDO

AFISA UHUSIANO MFUKO WA PESHENI WA PSPF, COLETA MNYAMANI AKITOA MAELEZO YA NAMNA YA KUJAZA FOMU YA UCHANGIAJI WA HIARI MOHAMED MUSSAALITPOTEMBELEA BANDA LA PSPF KWENYE MAONYESHO YA NANENANE MKOANI LINDI MWISHONI MWA WIKI
 BALOZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF, MRISHO MPOTO “MJOMBA”AKITOA BURUDANI KWA WAKAZI WA MKOA WA LINDI WALIOTEMBELEA BANDA LA PSPF WAKATI WA MAONYESHO YA NANENANE
BAADHI YA WANANCHI WA MKOA WA LINDI WAKIWA KATIBA BANDA LA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAKISHUHUDIA BURUDANI KUTOKA MJOMBA BAND

Sunday, August 10, 2014

MABONDIA MANENO OSWARD NA ABDALLA PAZI WAPIMA UZITO KUZIPIGA KESHO JUMAPILI MWANANYAMALA CCM MWIJUMA
Bondia Juma Biglee akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake kesho

 Bondia Abdallah Pazi akipima uzito kushoto ni Maneno Osward

Mabondia Maneno Osward kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumapili katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala jijini Dar es salaam picha zote na WWW.SUPESDBOXINGCOACH.BLOGSPOT.COM