b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, November 19, 2014

BASATA NA KITUO CHA UTAMADUNI CHA UJERUMAN (GOETH INSTITUT) WAENDESHA MAFUNZO KWA WASANII WA SANAA ZA MIKONO

Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza (Kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa batiki yaliyoanza mapema wiki hii kwenye Ofisi za Baraza hilo zilizoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni  Bi. Leah Ruhimbi

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla akiongea na Wasanii (hawako pichani) waliohudhuria kwenye mafunzo ya wiki moja ya utengenezaji batiki yanayoandaliwa na kituo chake kwa kushirikiana na BASATA na kufanyika makao makuu ya BASATA. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi akifungua mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi yanayofanyika kwa wiki moja makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba. Wengine kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua akiwaelekeza jambo wasanii wanaoshiriki mafunzo ya utengenezaji batiki 
Sehemu ya Wasanii wa utengenezaji batiki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
=======================================

Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ujeruman maarufu kama Goeth Insitut wameendesha mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za mikono yanayofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanayotazamiwa kudumu kwa siku tano yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa yanalenga kuongeza ubunifu na weledi miongoni mwa wasanii wa Sanaa za mikono ili kuongeza ubora na tija katika uzalishaji.  
Mapema akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Leah Ruhimbi alisema kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija kwa wasanii hao na kuwawezesha kubuni Sanaa zenye ubora zitakazopenya masoko mbalimbali ya Sanaa.
“Ni matarajio ya BASATA na wizara kwamba mafunzo haya yatakuwa yenye tija kwa wasanii na yatawawezesha kusambaza ubunifu na uzoefu kwa wasanii wengine nchini. Lengo ni kuwa na sanaa zenye ubunifu na ubora” alisisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Goeth Institut Bi. Eleonore Sylla alisema kwamba mafunzo hayo yanahusisha wasanii wenye uwezo wa kutengeneza batiki na lengo kuu ni kuwaweka pamoja ili wachangie uzoefu na baadaye kutengeneza batiki zenye ubora zaidi.
“Tunajua mnatoka sehemu mbalimbali nchini na wote mna uzoefu katika utengenezaji wa batiki lakini kuwa kwenu pamoja kwenye mafunzo haya kutawafanya mpate uzoefu zaidi na hatimaye kubuni batiki zenye ubora” aliongeza Sylla.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba BASATA kwa kushirikiana na Goeth Insitut wameona kwamba kuna haja ya mafunzo hayo ya wasanii na kwamba baraza litaendelea kuboresha ubora wa kazi za Wasanii kupitia kuwajengea uwezo.


No comments:

Post a Comment