b..

B1

Wynem

animation

Monday, December 8, 2014

RAIS KIKWETE APANGUA TENA WAKUU WA MIKOA


Jakaya Kikwete, president of Tanzania, answers questions at a press conference at the United Nations (UN) building in Addis Ababa, Ethiopia, during the 12th African Union (AU) Summit.
Rais Jakaya Kikwete

Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amempandisha cheo Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Daudi Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wengine sita wa mikoa kuanzia jana.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema Ntibenda ataapishwa leo, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Wakuu wa mikoa waliohamishwa ni Elaston Mbwilo anayetoka Manyara kwenda Simiyu kuchukua nafasi ya Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera anahamia Manyara kutoka Morogoro na nafasi yake inachukuliwa Dk Rajabu Rutengwe kutoka Tanga alikokaa kwa mwezi mmoja akitokea Katavi.
Magalula Magalula amehamishiwa Tanga kutoka Lindi ambako naye alikaa kwa mwezi mmoja akitokea Geita na nafasi yake inazibwa na Mwantumu Mahiza kutoka Pwani.
Mhandisi Evarist Ndiliko amehamishiwa Pwani kutoka Arusha alikohamia hivi karibuni kutoka Mwanza.
Katika taarifa yake, Balozi Sefue alisema wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Uhamisho huo umekuja ikiwa ni mwezi mmoja kamili tangu Rais Kikwete alipofanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa mikoa na kuwahamisha sita huku wengine watatu wakipangiwa kazi nyingine.
Wakuu wa mikoa wanne wapya ni Dk Ibrahim Msengi (Katavi), Amina Masenza (Iringa), Halima Dendego (Mtwara) na John Mongella (Kagera).
Kabla ya kuteuliwa, Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mwanza; Dk Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro na Mongela alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Walioachwa kwa ajili ya kazi nyingine ni Dk Christine Ishengoma (Iringa), Kanali Fabian Massawe (Kagera) na Kanali Joseph Simbakalia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ambaye tayari ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Sorce- gazeti la Mwananch 08/12/2014

No comments:

Post a Comment