b..

B1

Wynem

animation

Thursday, June 11, 2015

JANUARI MAKAMBA AVUNJA REKODI YA UDHAMINI NA MAPOKEZI IRINGA

Mh. January Makamba akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi Jesca Mambatavangu mara baada ya January kusaini kitabu cha wageni katika ofisi za Chama.

Mchngaji Kiwanga wa Iringa mjini akimkaribisha Mh. January Makamba na Mkewe katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa. Mchngaji huyo alimwombea na kumpa baraka zote za kugombea nafasi ya urais kupitia CCM.

Baadhi ywa wanachama wa Waendesha Bodaboda waliojitokeza kumpokea na kumsapoti  Mh. January Makamba katika zoezi lake la kusaka wadhamini ndani ya chama ili aweze kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi. 

Mh. January Makamba na Mkewe wakisalimiana na baadhi ya vijana na wanachama wa CCM mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wiliya ya Iringa Mjini.

Mh. January Makamba na Mkewe wakiwapungia mkono baadhi ya vijana na wanachama wa CCM waliofika kumsapoti mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wiliya ya Iringa Mjini.

Mh. January Makamba akiweka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa Mjini. Aliyesmama kulia kwake ni Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Zongo Lobe Zongo na kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Abeid Kiponza.

Mh. January Makamba akipunga Mkono kwa wanachama wa Iringa waliokuja kumuunga mkono mara baada ya kutoka kuewka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa Mjini.

Badhi ya vijana wa Iringa waliohuria katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Mjini wakimsikiliza Mh. January Makamba huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofautitofauti.

Mh. January Makamba na Mkewe wakiimba pamoja na wanachama wa CCM waliojitokeza katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Mjini katika kumsapoti na kumdhamini kumuwezesha kushinda katika kinyang'anyiro cha kupewa ridhaa ya kugombea urais kupita CCM.

Mh. January Makamba akikabidhiwa fomu yenye majina ya wanachama waliomdamini na Mwenyekiti wa CCM wilya, Abeid Kiponza.  Fomu hiyo in idadi ywa wanachama 630 waliojitokeza kumdhamini ikiwa ni kutoka wilaya ya Iringa Mjini na Kilolo.

Mh. January Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM wilaya ya Iringa Mjini walijitokeza kumsapoti na kumdhamini. January amepata sahihi 630 za wanachama wa CCM kumdhamini, idadi hiyo ni ya wilaya ya Iringa Mjini na wilaya ya Kilolo. Picha Zote na Mpigapicha Wetu.

No comments:

Post a Comment