b..

B1

Wynem

animation

Saturday, October 31, 2015

WIZ KID AZUNGUMZIA SHOO YAKE YA LEO USIKU

Msanii Wiz Kid akiwasili katiktika viwanja vya ukumbi wa Solomins kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa Habari
Msanii Wiz Kid akisalimiana na Mratibu wa Tamasha la msanii huyo, King Solomins
Msanii Wiz Kid akitembea kuelekea ndani ya ukumbi wa Solomins kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa Habar
Mratibu wa Tamasha la Wiz Kid, King Solomins akizungumza na waandishi wa Habari akielezea kuhusu shoo nzima ya Wiz Kid itakayofanyika leo katika Viwanja vya Leaders Club.
Msanii Wiz Kid akizungumza na waandishi wa Habari akielezea kuhusu shoo nzima atakayoifanya leo usiku katika Viwanja vya Leaders Club.
Picha zote na Sule Junior

Friday, October 30, 2015

Wapigaji vyombo wa WizKid wawasili

Wakiingia katika basi tayari kwa msafara
Watumiaji mbalimbali wa vyombo vya muziki wa msanii Wizkid wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere tayari kwa shoo yao ya leo katika Viwanja vya Leaders.
Huyo mwenye fulana nyeusi anaitwa  Snipes ndio kiongozi wa bendi ya msanii Wizkid
Wakiwa Uwanjani hapo ambapo wameahidi kufanya shoo kubwa wakishirikiana na msanii huyo.  

Wednesday, October 14, 2015

WATOTO YATIMA WA KITUO CHA VALENTINE CHILDREN HOME WAPIMWA AFYA ZAO

watoto wakiwa katika folerni ya kupimwa afya

Muhudumu wa afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha alafa kilichopo tandika Dar es salaam Bi, Latifa Masasi wa pili   mpima mtoto Nuru Edward wa kituo cha kulea watoto yatima cha Valentine children home kilichopo yombo buza kulia ni mtoto Clara Olimpia nae akihudumiwa na nesi Mary Hongoli


Muhudumu wa afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha alafa kilichopo tandika Dar es salaam Bi, Latifa Masasi wa pili akimpima afya mtoto Lovenes Masawe kulia ni nesi Mary Hongoli

watoto waliojitokezwa kuletwa kwa ajili ya kupima afya na wazazi wao wakiwa katika foleni ambapo jumla ya watoto waliojitokeza ni 230 ambao waliudumiwa na kupewa ushauli wa bule

Saturday, October 10, 2015

Aunt Ezekiel: Stukeni, hakuna mabadiliko bila kufanya kazi


 Na mwandishi Wetu
Watanzania hasa vijana wameshauriwa kuyafikiria kwa umakini mabadiliko wanayoyataka kabla ya kuchukua maamuzi wanaytaka kuchukua, hali itakayopelekea kuwa na umakini watakapofikia siku ya kupiga kura, siku ambayo wanapaswa kufanya maamuzi yaliyp sahihi.

Hayo yamesemwa na msanii wa filamu Aunt Ezekiel ambaye yupo katika kundi la kampeni la Nimestuka linalomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk John Pombe Magufuli, ambalo linafanya ziara za kijiji kwa kijiji kuwahamasisha vijana kukipigia kura Chama cha Mapinduzi ili kirudi madarakani kuendelea na utekelezwaji wa ilani yake ya uchaguzi.

Aunt amewaambia wakazi wa Malunga, Shinyanga, wasidanganywe na bei za bidhaa kwamba zimepanda sana ukilinganisha na miaka kumi iliyopita. Hizi bei pia zisingeweza kuwa zile zile kwa miaka kumi, hata wao wangekuwa wafanyabiashara wangepandisha tu.

"Mabadiliko bila na wewe kama kijana kujishughulisha hayawezi kuja, itakuwa ni miujiza, na hii ndio sababu yangu ya msingi nikaamua kurudi kwenye chama cha Mapinduzi ambako mgombea wake anasisitiza vijana kufanya kazi", alifafanua Aunt Ezekiel.

Aunt ambaye alikuwa ni mmojawapo kati ya wasanii wanaoliunga mkono kundi la vyama vya siasa la UKAWA, ame3waambia vijana wa Malunda kwamba vyama vya upinzani, bado havijawa tayari kutawala kwa kuwa linatumia vibaya nguvukazi ya vijana.

"Kule tunafundishwa kulalamika tu, kupinga serikali, hatuambiwi tufanye nini maisha yetu yawe bora, hatuambiwi kuhusiana na kuanzishiwa miradi, hii sio busara hata kidogo
 StanBakora, mmoja kati ya wasanii walio katika ziara ya Kijiji kwa Kijiji ya Nimes'tuka, akiongea mbele ya hadhara Shiyanga mjini
 Mboto naye akimwaga Pipi kwa wakazi wa Malunga
 Miss Tanzania Lilian Kamanzima, naye pia alitoa ujumbe wake 
 Umati wa wananchi wa Shinyanga mjini waliojitokeza katika mkutano wa kundi la Nimestuka uliofanyika katika kata ya Malunga

 Kitale akiingia uwanjani kwa ajili ya kuongea na wananchi wa Malunga...
Inspekta Haroun, ..Babu

Friday, October 9, 2015

TIMU NIMESTUKA WAWASTUA WATTU WA KAHAMA MJINI

Msanii ray Kigosi akimwaga sera kwa wananchi wa kahama mjini.
Msanii Ndende akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM kata Malunga jimbo la Kahama mjini mara baada ya kuwasili eneo la Tukio.
Msanii Skyner Ally akizungumza na wana Kahama.
Msanii, Kupa  akizungumza na wana Kahama.
Msanii, Sajent  akizungumza na wana Kahama.
Msanii, Mboto akiteremka garini 
Msanii, Mboto  akizungumza na wana Kahama.
Miss Tanzania 2014/2015,  akizungumza na wana Kahama.
Msanii Aunt Ezekiel  akizungumza na wana Kahama.
Msanii, Stan Bakora  akizungumza na wana Kahama.
Msanii, Kitale  akizungumza na wana Kahama.
Baadhi ya umati wa wananchi wa Kata ya Maluga jimbo la kahama mjini waliohudhuria mkutano huo.
Msanii, Inspector Harun  akizungumza na wana Kahama.

NEW HIT TRACK: KINGKAPITA FT. CANNIBAL - VIZABIZABINA


Wednesday, October 7, 2015

Ray Kigosi awastua Kishapu, awaambia upinzani bado sana

Na Mwandishi Wetu
Msanii Nguli wa filamu nchini, Ray Kigosi, amewaambia watanzania leokuwa makini na kusikiliza sera na kuachana na mihemko ya kisiasa itakayopelekea wao kufanya maamuzi watakayoyajutia baadae.

Kigosi ameyasema hayo alipokuwa katika moja ya mikutano inayoendeshwa na kundi la wasanii lenye kauli mbiu ya Nimestuka, katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kundi hilo inayopita kijiji kwa kijiji katika kuhakikisha kwamba wanawaelimisha vijana wenzao kuhusiana na usikilizwaji wa sera na mapokeo ya demokrasia kwa jamii.
Awali akiongea kabla ya kuwakaribisha wenzake 12 alioandamana nao, Kigosi amesema yeye alipokuwa Ukawa alikuwa akishuhudia vijana wakihamasishwa kupinga hata mambo yanayoonekana kuwa na tija yaliyofanywa na seriikali jambo ambalo yeye mwenyewe aliliona kuwa ni upotoshwaji wa wazi wazi.
"Naamini kuwa mpinzani, sio kupinga kila kitu, walipaswa pia kutufundisha jinsi ya kukabiliana na maisha kama vijana, lakini nikaja kugundua nimekosea sana kuacha kuungana mkono na Magufuli", alikiri Kigosi.
PICHANI JUU: Msanii wa filamu Ndende, akihamasisha wananchi wa Kishapu  kuhusiana na kumuunga mkono mgombea wa Chama cha Mapinduzi, Dk John Pombe Magufuli
Mchekeshaji Kitale, akiongea katika Mkutano wa Kampeni ya Nimes'tuka, inayoendeshwa na wasasnii wa filamu na muziki wa kizazi kipya, uliofanyika katika jimbo la Kishapu jioni hii
Inspekta Haroun, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya akitoa burudani kwa wakazi wa jimbo la Kishapu baada ya mkutano wao wa kampeni ya Nimes'tuka, inayoendeshwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, wanaokiunga mkono Chama cha Mapinduzi
Muigiza filamu maarufu, Kajala Masanja, akiongea katika mkutano wa kampeni za Nimes'tuka, uliofanyika katika jimbo la Kishapu mchana wa leo, kulia ni Ray Kigosi
Mchekeshaji Mboto, naye ni mmoja kati ya wasanii wanaoendesha kampeni za Nimes'tuka, hapa akiongea na wananchi wa jimbo la Kishapu, mkoani Shinyanga
Muigizaji Skyner Ally naye akimwaga sera zake katika kampeni za Nimes'tuka
Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima, akiongea na wananchi wa jimbo la Kishapu jioni ya leo katika mkutano wa kampeni za Nimes'tuka
Mikono juu...
Ray Kigosi akimwaga sera...
Msanii wa vichhekesho, StanBakora naye akiongea yake Kishapu leo